Dar es Salaam. Upo uhusiano kati ya uuzwaji wa dawa feki na kuwepo kwa maduka ya dawa ambayo ni bandia. Kama duka halijasajiliwa, nani anafwatilia kujua kama dawa inayouzwa hapo dukani imesajiliwa? Ukubwa wa tatizo barani Afrika Kwa sasa, takribani asilimia 10-15 ya dawa zinazosambazwa duniani kote ni dawa bandia. Usambazaji wa dawa hizi ni mkubwa zaidi barani Afrika, [Soma Zaidi]
Hujaandikiwa dawa? Hamna shida
Dar es Salaam. Sio kila homa ni Malaria, nenda ukapime. Bila shaka maneno haya sio mageni kwa watanzania wengi kwani yamewahi kuwa wimbo wa kampeni ya kitaifa katika kuwahimiza watu wasiwe na tabia ya aidha kwenda kujinunulia dawa kwenye duka la dawa bila kwenda kwa daktari, na hivyo kutibu ugonjwa ambao pengine sio ambao wanaumwa na wanaopaswa kuutibu. Ukisikia kichwa [Soma Zaidi]
Je, wanawake wa Tanzania wanajifungulia wapi?
Dar es Salaam. Kumekuwa na jitihada nyingi za serikali na wadau mbalimbali kuboresha miundombinu ya afya na kuwahamasisha akina mama kujifungua katika vituo vya matibabu ili kupunguza vifo vya akina mama na watoto vitokanavyo na uzazi. Hili ni moja ya malengo 17 ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ambayo yanatarajiwa kufikiwa mnamo mwaka 2030, yaani kupunguza vifo [Soma Zaidi]
Dawa zinanunulika?
Dar es Salaam. Mariana Hinju (35), anakumbuka jinsi ambavyo alimuuguza mama yake mwaka mmoja uliopita. Hinju, ambaye ni mama wa watoto wanne, alimleta mama yake kutoka Bukoba ili apate huduma nzuri ya matibabu ya macho. “Mama alikuwa na mtoto wa jicho. Ilibidi afanyiwe upasuaji kwenye macho yote mawili. Kwahiyo nikamleta Dar es Salaam ili apate huduma nzuri,” alisema Hinju. [Soma Zaidi]
Usiombe kuwa mgonjwa katia mikoa hii mitano Tanzania
Dar es Salaam. Changamoto za kupata huduma za matibabu zipo kila mahali nchini Tanzania. Kwa kutumia nyenzo mbalimbali kama tafuta vituo vya afya , iliyotengenezwa na shirika la Code4Africa, wananchi unaweza kujua kama kuna kituo cha hudua za afya karibu yao. Hata hivyo, yapo maeneo ambayo yana matatizo kuliko mengine. Katika mikoa mitano ambayo ina uhaba wa vituo vya afya, [Soma Zaidi]