• Habari
  • Ajira
  • Picha
  • Video
  • Data
  • Mwananchi.AfyaYangu

Afya Yangu na Mwananchi

Je, dawa uliyonunua ni bandia?

May 22, 2018 by Esther Karin Mngodo Leave a Comment

Dar es Salaam. Upo uhusiano kati ya uuzwaji wa dawa feki na kuwepo kwa maduka ya dawa ambayo ni bandia. Kama duka halijasajiliwa, nani anafwatilia kujua kama dawa inayouzwa hapo dukani imesajiliwa?

Ukubwa wa tatizo barani Afrika

Kwa sasa, takribani asilimia 10-15 ya dawa zinazosambazwa duniani kote ni dawa bandia. Usambazaji wa dawa hizi ni mkubwa zaidi barani Afrika, Asia, na Amerika ya kusini, ambapo asilimia 30 hadi 60 ya dawa ni bandia. Utafiti unaoangalia Malaria kama uhalifu dhidi ya ubinadamu, unaeleza kuwa taarifa ya Interpol inaonyesha kuwa asilimia 30 ya dawa za Malaria barani Afrika hazina viwango vya ubora unaotakiwa, au ni bandia. Kuwepo kwa dawa feki kunachangia watu kukosa imani na huduma za afya, kuongezeka kwa usugu wa dawa, na hata kifo. Shirika la Afya duniani WHO linaeleza kwamba watu 100,000 hufa barani Afrika kila mwaka kwasababu ya matumizi ya dawa bandia.

Taarifa ya The East African inaeleza Niger imewahi kuwa na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo katika miaka ya hivi karibuni. Chanjo zilizopelekwa wakati wa mlipuko huo, zilikuwa bandia. Ugonjwa huu hatari huua maelfu ya watu kila mwaka.

A report on The East African reported that Niger has had an outbreak of thyroid fever in recent years. Vaccines transmitted during the blast, were fake. This dangerous disease kills thousands of people each year.

Mwaka 2015, Shirika la kimarekani linalohusu madawa ya ukanda wa Tropiki na Usafi, lilisema kuwa watoto 122,000 wenye umri chini ya miaka mitano kwenye nchi za ukanda wa kusini mwa jangwa la Sahara, hufa kwasababu ya kumeza dawa za Malaria zisizo na kiwango kinachostahili.

Uelewa wa wananchi

Je, ukienda kununua dawa kwenye duka la dawa, unaweza kujua kwamba hii dawa ni bandia au la kwa kuiangalia? Utafiti ulioangalia uelewa wa watu kuhusu dawa feki na uwezo wa kutambua dawa feki za Malaria nchini Tanzania, uliochapishwa mwaka 2016, unaonyesha kuwa uelewa wa watu juu ya dawa za Malaria zilizo bandia, hasa za Malaria uko juu, hasa kama una taaluma ya afya.

Utafiti huu ambao ulihusisha washiriki 293, ulibaini kuwa asilimia 55.6 ya washiriki waliweza kutambua dawa feki, wakati asilimia 44.4 ya washiriki walishindwa. Hata hivyo, wengi waliokuwa na taaluma ya afya (asilimia 84) waliweza kutofautisha dawa feki na ambayo siyo feki. Tunaona jinsi kuwa na elimu ya maswala ya afya kunavyochangia uelewa na uwezo wa kutofautisha kilicho cha kweli na kilicho feki, kwani utafiti unaonyesha kuwa washiriki waliokuwa na uelewa na madhara ya kumeza dawa feki walikuwa na uwezo wa kutofautisha dawa, mara tatu zaidi ya wale ambao walikuwa hawajui nini madhara ya dawa hizo.

Vyombo vya habari vina mchango mkubwa wa kuelimisha jamii kuhusu dawa feki. Asilimia 68.9 ya washiriki wa utafiti huu walioweza kupambanua, walisema kuwa walipata elimu hiyo kupitia vyombo vya habari; huku asilimia 4.1 ya washiriki wakisema kuwa walijifunza kutoka kwa mtaalamu wa maswala ya afya.

Media plays an important part in educating the community about fisheries. Percentage of 68.9 per cent of the survey participants, said they received access to information through the media; while 4.1 percent of respondents said they had learned from a healthcare professional.

Taarifa ya DW inaeleza kuwa utafiti wa WHO wa hivi karibuni unaeleza kwamba kuna aina mbili ya dawa feki. Aina ya kwanza ni zile ambazo zilikuwa na hitilafu wakati wa kutengeneza, hivyo kuwa na upungufu katika hali ya ubora. Halafu, aina ya pili ni dawa ambazo toka zinatengenezwa, ni bandia.

Mzigo wa kiuchumi

Uuzwaji wa dawa bandia ni mzigo wa kiuchuni barani Afrika. Ripoti inayoangalia madhara ya kiafya na kiuchumi ya madawa bandia barani Afrika, inaeleza kuwa uuzwaji wa dawa feki kunaondoka soko la dawa halali. Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2009 inaeleza kuwa mauzo ya dawa milioni 45 bandia za Malaria, yalikuwa dola za kimarekani milioni 438, ambayo ni zaidi ya pato la taifa la nchi ya Guinea-Bissau. Huko nchini Kenya, ripoti zinaonyesha kuwa dawa bandia ni sawa na asilimia 40 ya dawa zinazouzwa nchini humo. Hii ni sawa na kiasi cha dola za kimarekani 130 kwa mwaka.

Kwa upande mwingine dawa bandia na bidhaa zingine zote bandia hukwepa ulipaji kodi, na hivyo kuathiri ukusanyaji wa mapato, na ukuaji wa pato la taifa. Kwa nchi za Afrika Mashariki (Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda), uuzwaji wa bidhaa bandia, ikiwemo madawa, huchangia ukwepaji kodi ya zaidi ya dola za kimarekani milioni 500. Nchini Tanzania, kiasi cha kati ya dola za kimarekani milioni 370 na 617 hupotea kwa mwaka kwasababu ya ukwepati kodi kunakochangiwa na uuzwaji wa bidhaa bandia, ikiwemo madawa.

Dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi (ARV)

Kumekuwa na hali ya taharuki miaka ya nyuma, hususani mwaka 2012 pale ambapo vyombo vya habari viliripoti kuwa kulikuwa na dawa bandia za kufubaza makali ya vvu (ARV) sokoni. Wadau mbalimbali, wakiwemo SIKIKA walipongeza serikali kwa hatua hiyo. Waziri wa Afya wa wakati huo Dr Hussein Mwinyi alilifungia shirika la Tanzania Pharmaceutical Industries Limited (TPI) kilichozalisha dawa hizo. Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam wa wakati huo, ambaye pia alikuwa Afida Mtendaji Mkuu TPI Ramadhan Madabida alifikishwa mahakamani na kesi bado inaendelea.

Jitihada za serikali

Pamoja na kwamba kiujumla bado hali siyo nzuri sana, serikali imekuwa ikifanya jitihada kubwa kukabiliana na changamoto hii. Hivi karibuni, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alitoa rai kwa wataalamu kuisaidia serikali kupambana na tatizo hili la kitaifa. Na  kumekuwa na kamata kamata ya madawa feki pamoja na bidhaa zingine, inayofanywa na shirika la kudhibiti vyakula na madawa (TFDA) kama operesheni endelevu. Na hata kufikisha mahakamani watu wanaohusika na usambazaji wa madawa bandia. Cha kushangaza, mkoa wa Mbeya umekuwa na sifa ya kuingiza vipodozi bandia kwa wingi zaidi nchini.

Pia, TFDA inaripoti kufurahishwa na ubora wa dawa kwa zaidi ya asilimia 95 baada ya kuweka miundombinu ya kufuatilia madawa yanapoingia sokoni. Kutoka wafanyakazi 53, hadi 300 walioko sasa, shirika hilo linaongeza juhudi za kukabiliana na tatizo.

TFDA pia ilizidua Maabara Hamishika (Minilab kit) mpya kumi Oktoba 2017, kama nyongeza, ili kuimarisha udhibiti wa ubora na usalama wa dawa kabla na baada ya kuingia katika soko la Tanzania. TFDA imekuwa ikitekeleza mpango wa upimaji wa awali (screening) wa dawa za kifua kikuu, dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARVs), malaria pamoja na vijiua sumu (antibiotics) kwa kutumia Maabara Hamishika (Minilab kits) katika vituo vya forodha na baadhi ya hospitali za mikoa tangu mwaka 2002. Uwepo wa Maabara Hamishika hamishika sokoni umesaidia kupunguza dawa zisizo na viwango kutoka asilimia 3.7 mwaka 2005 hadi asilimia 1 mwaka 2017. TFDA ilitenga fedha kiasi cha TZS 100 milioni katika bajeti ya mwaka 2016/17 kwa ajili ya ununuzi wa Maabara Hamishika nyingine 10 na hivyo kufanya idadi ya maabara hizi sasa kufikia 25 kutoka 15 mwaka 2012/13.

 

Filed Under: Uncategorized

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recent Posts

  • Afya ya uzazi wa mpango yapata pigo kwa punguzo la bajeti
  • Je, dawa uliyonunua ni bandia?
  • Hujaandikiwa dawa? Hamna shida
  • Je, wanawake wa Tanzania wanajifungulia wapi?
  • Dawa zinanunulika?

Recent Comments

    Archives

    • June 2018
    • May 2018

    Categories

    • Dawa
    • Uncategorized

    Meta

    • Log in
    • Entries feed
    • Comments feed
    • WordPress.org

    Mwananchi Communications Ltd is a multimedia company and publisher of Tanzania’s leading daily Kiswahili newspaper Mwananchi and Mwananchi Jumapili, its Sunday edition.

    The Health Portal is a collaboration between Mwananchi and Code for Tanzania, a civic tech and data-journalism initiative, part of a continent-wide Code for Africa project.

    Other Projects:
    • HURUmap Tanzania
    • Open Data TZ
    • The Citizen My Health
    • Mwananchi Data Portal

    Join our community:
    • HacksHackers Africa

    Copyright © 2023 · Magazine Pro Theme on Genesis Framework · WordPress · Log in